Wednesday, 6 May 2009

Mengi vs Rostam;who is fooling who?!

Naam hili nalo limetokea,linaendelea kuchukua sura mpya kila uchao, na kila mmoja analitazama kwa mtazamo wake.

Naongelea malumbano yanayoendelea kati ya Mfanyabiashara maarufu Reginald Mengi na mfanyabiashara mwingine aliye pia mwanasiasa-mbunge wa Igunga- Rostam Aziz juu ya kushutumiana kuhusu ufisadi.

Wengi wetu tumekuwa watazamaji katika hili. Hatahivyo katika utazamaji huu, kila mmoja aliyeweza kuongea la kwake amefanya hivyo. Hii ni kwasababu yale wanayoyaongea wawili hawa yanaigusa kwa namna moja au nyingine jamii ya Kitanzania.

Wengi wetu-kama si wote hatujui nani hasa ni mkweli kati ya hawa wote. Hatahivyo kuna maswali kadhaa ya kujiuliza katika hili:

1. Hawa wote wawili walikuwa wapi kushutumiana siku nyingi kabla ya sasa?nini kimepelekea kuinuka hivi sasa na kunyosheana vidole?

2. Je,vyombo husika vya dola vimechukua hatua gani mpaka sasa kushughulikia shutuma hizo kutoka kila upande?kama havijafanya hivyo,ni kwanini?

3. Je,vyombo vya habari- iwe vinavyomilikiwa na wanaoshutumiana ama la-vimewajibika kwa uadilifu katika kuifahamisha jamii kuhusu malumbano haya?

4. Je, taifa kwa ujumla linafaidika au linaathirika vipi hasa katika malumbano haya?

Kwa maswali haya machache na mengine mengi yaliyomo vichwani mwa watu-hatua hitajika zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya malumbano haya.

Tutafakari- wanaohusika wachukue hatua.
Wadau mnasemaje?

1 comment:

  1. These guys are taking up a lot of space in Television airtime and newsapers, the space and time that could have been used productively to advance other causes and address important issues facing our country. Editors in both, print and electronic media are partly to blame. They are letting us down by failing to play their role as "Gate Keepers" who decide what is "newsworthy" and what is not.

    Mind you, these people are both media owners. They both own newspapers and Television stations. I think it is high time the government should address the issue of media ownership.

    These fracas are just part of the detrimental effects of concentrated media ownership. Where is MCT?

    Deo, bizeyes.blogspot.com

    ReplyDelete